Freddy ilipiga eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja mwishoni mwa juma na bado ilikuwa ikisababisha mvua kubwa Jumatano, na kutatiza juhudi za kutoa misaada.
Mimi binafsi nimehuzunishwa sana Chakwera aliwaambia waandishi wa habari katika kitongoji cha Chilobwe cha Naotcha, nje kidogo ya mji wa Blantyre. Wakati mwingine unapopita nje na kuona majeneza mengi hivi huwezi kujizuia kutoa machozi kwa sababu wapendwa familia nzima imefutiliwa mbali na wengine wengi ambao wameguswa.
Idara ya usimamizi wa majanga nchini Malawi imesema katika taarifa yake kwamba idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga hicho cha pili imeongezeka hadi 225 kutoka 190 huku watu 707 wakijeruhiwa na wengine 41 hawajulikani waliko.