Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kwamba mazungumzo hayo ya wiki moja, yaliyoanza leo Jumanne yatakamilika Jumapili.
Mazungumzo yanaongozwa na Umoja wa Afrika, ni ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya wanajeshi wa serikali kuu ya Ethiopia na wapiganaji wa Tigray, miaka miwili iliyopita.
Serikali ya Afrika Kusini imesema kwamba ipo tayari kuwa mwenyekiti wa mazungumzo ya amani ya Ethiopia na kutoa msaada wowote utakaohitajika.
Msemaji wa rais Ramaphosa, Vincent Magwenya, amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali ya Afrika Kusini ina matumaini kwamba mazungumzo hayo yatapelekea kupatikana kwa amani ya kudumu kwa watu wa Ethiopia.