Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 01:04

Ethiopia imetia saini mkataba wa muundo wa uwanja mpya wa ndege


Shirika la ndege la Ethiopian
Shirika la ndege la Ethiopian

Uwanja huo utakuwa karibu na mji wa Bishoftu takribani kilomita 45 kutoka mji mkuu Addis Ababa

Ethiopia imetia saini mkataba kwa muundo wa uwanja mpya wa ndege wenye njia nne ambao wakati ujenzi utakapokamilika mwaka 2029 utakuwa ni mkubwa sana Afrika, Mkuu wa shirika la ndege la Ethiopia linalomilikiwa na serikali amesema Ijumaa.

Uwanja huo utakuwa karibu na mji wa Bishoftu takribani kilomita 45 kutoka mji mkuu Addis Ababa, utakuwa na uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni 100 kwa mwaka na kutoa maegesho 270 ya ndege, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege la Ethiopia, Mesfin Tasew aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Kampuni ya Sidara inayohusika na uhandisi na ushauri yenye makao yake Dubai, itachora muundo wa uwanja huo wa ndege, mkurugenzi anayesimamia operesheni za kampuni hiyo, Tariq Al Qanni alisema. Mipango ya kujenga uwanja wa ndege ilitangazwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Mesfin alisema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Addis Ababa, ambao kwa hivi sasa ni kitovu kikuu cha shirika hilo kubwa la ndege barani Afrika, hivi karibuni utafikia uwezo wa kuhudumia abiria milioni 25 kwa mwaka. “Ni mradi wa miaka mitano ambao utakamilika mwaka 2029. Utakuwa mkubwa zaidi barani Afrika, Mesfin alisema.

Forum

​
XS
SM
MD
LG