Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:35

El Nino yaangaziwa kuathiri Africa Mashariki na Kusini


Na mwaka 2015 unatarajiwa kuwa mwaka mwengine mbaya wa El Nino, anasema Bw. Ruirie.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:43 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Idara ya watoto ya umoja mataifa inaonya kwamba takriban watoto millioni 11 huko Afrika mashariki na kusini wako hatarini kutokana na njaa, magonjwa na upungufu wa maji kutokana na hali ya mfumo wa hali ya hewa ujulikanao kama El Nino kupata nguvu Zaidi. Kenya na Uganda zinajitarisha kwa mafuriko, wakati Afrika kusini na Malawi tayari wanakumbana na ukame.

Onesmus Ruirie, mtaalam mkuu wa hali ya hewa kwenye idara ya hali ya hewa nchini Kenya, anakumbuka pale El Nino ilipoathiri Kenya hapo mwaka 1997 na 98. Hio ilizingaatiwa kama mfumo mkubwa zaidi wa El Nino kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1950 pale wanasayansi walipoanza kuweka rekodi za kuaminika za uchunguzi.

Ruirie anasema kulikuwa na mvua nyingi kote nchini, ambayo ilipelekea uharibifu wa miundo mbinu, mafuriko, magonjwa, na kupotea kwa maisha ya watu. Kwa hiyo mwaka 1997 ulikuwa mwaka mbaya wa el Nino.

Na mwaka 2015 unatarajiwa kuwa mwaka mwengine mbaya wa El Nino, anasema Bw. Ruirie.

El Nino ni kuwa na ujoto kwa maeneo ya kati na Equitorial ya bahari ya Pacific. Inatokea takriban kila miaka 2 hadi 7, na inaweza kuwa na athari kubwa kwa hali ya hewa kote duniani. Hayo ni kwa mujib wa Tom Di Liberto, mtabiri wa hali ya hewa katika kiuo cha National Oceanic and Atmospheric administration NOAA mjini Washington DC.

Bw. Di Liberto anasema, ukiona tempreture za bahari zikiongezeka joto, inaweza kubadilika kutegemea na jinsi hali ya anga inavyofanya kazi kwenye tropiki, na inaweza kupelekea athari mbali mbali na kuathiri hali ya hewa na mifumo ya hali ya hewa hata sehemu za mbai kutoka hapo bahari ya pacific tu.

Wakati wa matukio ya El Nino, nchi za Afrika mashariki hupata mvua nyingi, nan chi za kusini mwa Afrika pamoja na Australia na Indonesia, hupata ukavu na ukame na mioto ya misitu.

Lakini utabiri dio daima kuwa ukweli. Hapo mwaka 1997 kwa mfano, hali ilitarajiwa kuwa kavu huko kusini mwa Afrika, lakini hilo halikutokea.

Japo El Nino husababisha uharibifu, lakini el Nino nayo pia ina manufaa yake.

Di Liberto anasema mwaka huu unaweza kuwa mfumo thabiti Zaidi wa el Nino kuwahi kurekodiwa, lakini anasema, hilo haliwezi kuamuliwa hadi mapema mwaka ujao, pale takwimu zote zimetathminiwa.

XS
SM
MD
LG