Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:43

Wamisri wapiga kura za wabunge


Wamisri wengi wamejitokeza kwenye vituo vya kupigia kura huko Giza, Misri, Disemba 14, 2011.
Wamisri wengi wamejitokeza kwenye vituo vya kupigia kura huko Giza, Misri, Disemba 14, 2011.

Raia wa Misri leo wamejitokeza kwa mara nyingine kupiga kura za wabunge katika majimbo yao

Wamisri walijitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura katika theluthi moja ya majimbo ya nchi hiyo Jumatano, ambapo ni mzunguko wa pili wa uchaguzi wa wabunge nchini humo, huku vyama vya ki-Islam vikiwa na matumaini ya kuongeza nguvu zao katika uchaguzi.

Upigaji kura ulifanywa katika maeneo tisa, Jumatano yakiwemo maeneo ya Aswan, Beni Suef, Giza, Ismailia, Suez na Sohag. Zaidi ya wamisri milioni 18 wanastahiki kupiga kura katika mzunguko wa pili ambao unamalizika Alhamisi.

Wapiga kura wanachagua wabunge watakaowawakilisha katika majimbo yao kutoka idadi ya wabunge 498. Kundi la Muslim Brotherhood Freedom and Justice Party na kundi jingine la kihafidhina la al-Nour Salafi Islamist walishinda katika mzunguko wa kwanza wa upigaji kura uliofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba.

Baadhi ya nchi za Magharibi zina wasi wasi kwa vyama vya ki-Islam kushika nafasi ya mbele. Lakini baadhi ya waislam wanaelezea wasi wasi wao wenyewe , wakionya dhidi ya itikadi za uhuru wa magharibi, kama vile ndoa za mashoga, kuvutia wapiga kura katika maeneo ya vijijini.

Mzunguko wa tatu wa uchaguzi unajumuisha majimbo tisa yaliyobaki, ambayo yatapiga kura mwanzoni mwa mwezi Januari.

Uchaguzi wa wabunge ni wa kwanza kufanyika nchini Misri tangu kuzuka kwa ghasia maarufu zilizomuondoa madarakani Rais wa zamani Hosni Mubarak.

Uchaguzi wa wawakilishi katika bunge dogo utaanza mwishoni mwa mwezi Januari na kumalizika mwezi Machi, baada ya hapo bunge litaandika katiba mpya.

XS
SM
MD
LG