Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 01:54

Ecuador kutoruhusu Wachina kuingia nchini bila Visa


Ecuador inasema itasitisha kanuni ya kuingia nchini humo bila visa kwa raia wa China, kuanzia Julai 1, kwa kunyoshea kidole tatizo la ongezeko la uhamiaji usio wa kawaida.

Katika miaka michache iliyopita, Ecuador imekuwa mahali kwa kuanzia kwa maelfu ya raia wa China ambao wameamua kuchukua safari ndefu na ya hatari kupitia Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati na Mexico mpaka kufikia mpaka wa kusini wa Marekani.

Baadhi ya watu ambao tayari wamehamia Marekani wanasema uamuzi wa Ecuador na hatua inayokuwa ya Washington na Beijing kukomesha mtiririko wa uhamiaji haramu ni ishara kwamba mlango unaweza kufungwa kwa wale wanaotaka kufanya safari ya “zouxian” maarufu kama inavyofahamika kwa Kichina

Forum

XS
SM
MD
LG