Mkuu wa shirika la afya duniani WHO amesema Alhamisi kwamba ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi unaweza kuangamizwa kabisa kufikia mwisho wa mwaka huu. Kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Daktari Margaret Chan ameambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa uangalizi ulioko sasa na kushughulikia uwezo zaidi kumeimarika na wafanyakazi wa afya sasa wana ufahamu zaidi wa jinsi ugonjwa wa Ebola unavyoambukizwa.
Akizungumza kwa njia ya video kutoka Hong Kong, Dkt Chan amesema mataifa matatu ya Afrika magharibi yalioathiriwa zaidi yamepiga hatua kubwa. Kesi mpya zilizoripotiwa Liberia zimezuiwa huko Guinnea na Sierra Leone na ni jumla ya kesi tatu pekee zimeripotiwa kila wiki katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Hilo lina maana kuwa iwapo juhudi za kugundua na kufuatilia zitaongezwa, basi virusi hivyo vitakomeshwa kufikia mwishoni mwa mwaka.Yaani kufukia sifuri na kubaki kwenye sifuri. WHO inasema mlipuko mpya wa Ebola ulioanza mwaka jana hautatangazwa kuangamizwa rasmi hadi pale maambukizo yatakapokwisha na kufikia zero. Kumekuwa na karibu maambukizi 28,000 ya Ebola na zaidi ya vifo 11,000.