Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:29

Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete kuongoza wasimamizi wa uchaguzi Kenya


Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete

Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya imeendelea na mikakati ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofanyika mwezi huu.

Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete ataongoza kamati yenye wajumbe 52 nchini Kenya kama waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Kenya unatarajiwa kuanza Agosti 9.

Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi , Jakaya amesema wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kuwasilisha ripoti kuhusu uchaguzi huo ifikapo Agosti 11.

Kundi hilo linalenga kujua jinsi wadau mbalimbali wanaohusika na uchaguzi huu walivyojianda, kuendesha na kushiriki uchaguzi na pia kungalia jinsi shughuli za uchaguzi zinavyoendeshwa.

Ripoti zilizowasilishwa na waangalizi hutoa ukosoaji wa lengo la mchakato wa uchaguzi, kutoa mapendekezo kuhusu jinsi Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka inavyoweza kuboresha usimamizi wa siku zijazo.

Rais mstaafu Kikwete amekuwa akiongoza misheni ya waangalizi wa uchaguzi barani Afrika, ziara yake ya hivi karibuni ikiwa nchini Zambia ambako aliongoza timu inayowakilisha Jumuiya ya Madola.

XS
SM
MD
LG