Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:54

Prince William na mkewe wapata mtoto wa kike


Tony Appleton akitangaza kuzaliwa kwa mtoto wa kike wa kifalme nje ya hospitali ya St. Mary's Hospital, London, May 2, 2015.
Tony Appleton akitangaza kuzaliwa kwa mtoto wa kike wa kifalme nje ya hospitali ya St. Mary's Hospital, London, May 2, 2015.

LONDON - Mke wa mwana mfalme William, Kate amejifungua mtoto wa kike Jumamosi Mei 2 mjini London, maafisa wa ufalme wa Uingereza wametangaza.

Katika taarifa fupi Kensington Palace, makao makuu ya Ufalme wa Uingereza, ilitangaza kuwa Kate "amejifungua kwa salama mtoto wa kike" saa mbili na dakika 34 kwa saa za London, kiasi cha saa tatu baada ya kulazwa katika hospitali ya St. Mary's mjini London.

Prince William na mkewe Kate
Prince William na mkewe Kate

Tangazo hilo lilipokelewa kwa shangwe nje ya hospitali hiyo, ambapo mashabiki wa ufalme wakiwa wamevalia nguo za rangi ya bendera ya Uingereza wamekuwa wakipiga kambi kusubiri habari za kuzaliwa kwa mtoto wa pili wa Prince William na mkewe.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa paundi nane na pointi 3. Tangazo hilo lilisema pia kuwa Kate na mtoto wako katika afya nzuri na kwamba Prince William alikuwepo wakati wa tukio hilo.

Mtoto huyo - ambaye kifalme atajulikana kama princess, atakuwa wa nne katika urithi wa ufalme wa Uingereza nyuma ya babu yake Prince Charles, baba yake Prince William na kaka yake Prince George ambaye alizaliwa katika hospitali hiyo hiyo Julai 2013.

XS
SM
MD
LG