Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:20

DRC yashutumu Rwanda kwa kuweka vikwazo katika mazungumzo yanayoendelea kutatua mzozo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo akiwasili kuhutubia Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Septemba 20, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo akiwasili kuhutubia Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Septemba 20, 2023.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeishutumu Rwanda kwa kuweka vikwazo katika mazungumzo yanayoendelea kutatua mzozo wa waasi wa M23 mashariki mwa DRC ambao umesababisha zaidi ya watu milioni 1.7 kuyahama makazi yao.

Maoni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo Therese Kayikwamba Wagner kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne yanafuatia shutuma kutoka kwa mwenzake wa Rwanda kwamba Congo ilikataa kutia saini makubaliano yaliyokubaliwa mwishoni mwa Agosti kama sehemu ya mazungumzo ya amani

Kundi la M23 linaloongozwa na Watutsi limekuwa likiendesha uasi katika eneo la mashariki mwa Congo lililokumbwa na ghasia tangu mwaka 2022. Congo, Umoja wa Mataifa na mataifa mengine yanaishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuliunga mkono kundi hilo kwa majeshi yake na silaha.

Forum

XS
SM
MD
LG