Waasi wa ADF walishambulia raia katika vijiji viwili karibu na Komanda, umbali wa kilomita 75 na mji wa Bunia, amesema David Beiza, mkuu wa shirika la mslaba mwekundu katika wilaya ya Irumu mkoani Ituri.
Beiza amesema waasi hao walishambulia pia kijiji cha Mangusu ambapo raia 17 walifariki na kijiji cha Shauri Moya kulikouliwa watu 9. Ameongeza kuwa washambuliaji walilenga daraja kwenye mto Ituri na kuua watu wanne.
Kundi linalofuatilia masuala ya usalama DRC, Kivu Security Tracker ( KST), liliripoti baadaye kwenye Twitter kwamba watu 18 waliuawa Jumatatu katika kijiji cha Mangusu, na kuongeza kuwa ADF wanashukiwa kutekeleza mauaji hayo.