DRC inadai kwamba waasi wa M23 wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda, huku serikali ya Rwanda ikidai kwamba kundi la waasi la FDLR linaungwa mkono na DRC.
Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC Gen. Celestin Mbala, ametuma kikosi maalum mashariki mwa nchi hiyo kupambana na waasiwa M23.
Generali Mbala alikuwa mjini Goma wiki iliyopita kwa ziara ya kuthathmini oparesheni za wwanajeshi wa serikali dhidi ya kundi la M23.
DRC inadai kwamba waasi wa M23 wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda.
Akiwa mjini Goma, Mbale amesema kwamba Congo haitaacha hata ncha moja wa ardhi yake kwa waasi.
Baadaye alielekea Lubumbashi, ambao ni mji wa tatu kwa Ukubwa nchini Congo, na kufanya kikao na wanajeshi wa serikali namna ya kupigana na M23.
Uhusiano kati ya Rwanda na DRC
Mapigano makali yalitokea kati ya kundi la M23 na wanajeshi wa serikali wiki iliyopita, waasi wakiteka nyara kambi za wanajeshi wa serikali.
Mashambulizi mapya ya kundi la M23 yamepelekea uhusiano kati ya DRC na Rwanda kuharibika.
Wanajeshi wa DRC walitumia silaha nzito kukabiliana na waasi wa M23. Roketi za jeshi la DRC zilianguka Musanze ndani ya Rwanda, na kuikasirisha serikali ya Rwanda.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta, amesema kwamba rais Paul Kagame amezungumza na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi kwa njia ya simu na kusema kwamba Kigali ina haki ya kujibu mashambulizi dhidi yake yanayofanywa na jeshi la DRC.
DRC imedai kukamata wanajeshi wa Rwanda
DRC na Rwanda zimeeka idadi kubwa ya wanajeshi mpakani huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka.
Mnamo Jumamosi, wanajeshi wa DRC walionyesha waandishi wa habari wanajeshi wawili wa Rwanda ambao walikamatwa na jeshi la DRC, wakidaiwa kwamba walikuwa ndani ya mipaka ya DRC.
Rwanda inadai kwamba wanajeshi wake walitekwa nyara wakiwa wanapiga doria ndani ya mipaka ya Rwanda.
Uganda kusaidia Rwanda?
Kamanda wa jeshi la ardhini la Uganda Lt Gen Muhoozi Kainerugaba, aliandika ujumbe wa Twiter mwishoni mwa wiki iliyopita akisema kwamba kundi la waasi la Rwanda linalopigana mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo linastahili kuacha vita mara moja.
Muhoozi amesema kwamba hajawahi kupigana na kundi lnterahamwe, akiwa na maana y akundi la Democratic forces of liberation of Rwanda FDLR.
Muhoozi alisema kwamba amewapa waasi hao wiki chache kujisalimisha kabla ya kuwashambulia.
Kundi la waasi la FDLR
FDLR, ambalo ni kundi la wahutu linalopinga wa tutsi, ni moja ya makundi ya waasi yanayopigana vita nchini Congo.
FDLR ni kundi ambalo wanachama wake walisababisha mauaji ya kimbari yam waka 1994, nchini Rwanda.
Rwanda, ambayo inashirikiana na jeshi la Uganda kukabiliana na makundi ya waasi nchini DRC, imeshutumu maafisa wa DRC kwa kushirikiana na kundi la FDLR.
Shutuma hizo ambazo hazijaambatana na ushahidi wowote, zimeongeza hali ya mvutano kati ya DRC na Rwanda, ambazo zilipigana vita vikali miaka ya 1990, na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.
Jeshi la Rwanda RDF, limeshutumu wanajeshi wa DRC kwa kushambulia Rwanda kwa roketi, mnamo May 23.
Rwanda imeshutumu DRC
Serikali ya Rwanda imesema kwamba jeshi la DRC, FARDC na waasi wa FDLR, walishambulia jeshi la RDF kwenye mpaka wa DRC na Rwanda, na kuwateka nyara wanajeshi wawili wa Rwanda waliokuwa wanapiga doria mpakani.
Jeshi la DRC halijajibu shutuma za utekaji nyara, lakini maafisa wa serikali wameshutumu Rwanda kwa kusaidia waasi wa M23 kutekeleza mashambulizi katika sehemu kubwa yenye utajiri wa madini, nchini DRC.
Rwanda imesema kwamba wanajeshi waliotekwa nyara, Cpl Elysee Nkundabagenzi na Pte Gad Ntwari, wanashikiliwa na kundi la FDLR, mashariki mwa DRC.
Jeshi la Rwanda lilitoa taarifa iliyotaka maafisa wa DRC kuhakikisha kwamba wanajeshi wake wanaachiliwa haraka iwezekanavyo.
Haya yote yanajiri wakati jumuiya ya Afrika mashariki imeanza shughuli ya pamoja ya kijeshi, inayofanyika Uganda.
Jumla ya wanajeshi 150 na polisi 36 wa Rwanda wametumwa kushiriki mazoezi hayo ya 12 ya wanajeshi kutoka jumuiya ya Afrika mashariki kwa jina Ushirikiano imara 2922, yanayofanyika Uganda kuanzia May 27 hadi June 16 mwaka huu.
Mazoezi hayo ya wiki mbili yanaleta pamoja vikozi vya jeshi vya Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan kusini na Rwanda.
Juhudi za EAC kusuluhisha mgogoro wa DRC
Hivi karibuni, viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki walikutana Nairobi kenya na kukubaliana kuund ajeshi la pamoja kukabiliana na waasi mashariki mwa DRC.
Vyombo vy ahabari vya Ugand avinaripoti kwamba jeshi la Rwanda limeeka kambi ndani ya DRC kuzuia mashambulizi ya kundi la FDLR.
Ge. Muhoozi, ambaye alikuwa kamanda wa jeshi maalum la Uganda, amesema kwamba baada ya kumalizana na kundi la Allied democratic Forces ADF, ataanza mashambulizi dhidi ya FDLR.
Muhoozi amesisitiza kwamba kundi ambalo liliuwa “ndugu na dada zetu mwaka 1994, hakuna mda wa mazungumzo tena. Ujumber wa twiter wa Muhoozi, unaashiria kwamba Uganda itashirikiana na Rwanda kupambana na waasiw a FDLR, linaloshutumiwa kwa ukandamizaji wa haki za kibinadamu kivu kaskazini.
Muhoozi aliandika kwamba wapiganaji wote wa Interahamwe wanastahili kujisalimisha kwa kambi yoyote ya UPDF au RDF iliyo karibu nao na kwamba wameamua kuita opareshini dhidi yao kuwa Oparesheni dhidi ya Rudahigwa.
Ili kutekeleza Opareshini aliyozungumzia Muhoozi, Rwanda na Uganda zinastahili kupata idhini ya DRC. Uhusiano kati ya Kigali na Kinshahsa unaonekana kuharibika.
Rwanda imesitisha safari za ndege kuelekwa DRC, huku DRC ikisema kwamba itatangaza hatua za kulipiza kisasi.