Mvutano juu ya ratiba ya uchaguzi na kubadilishwa utaratibu wa uchaguzi umeisababisha tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemnokrasia ya Kongo, CENI kutoweza kutangaza siku ya uchaguzi.
Uwamuzi huo umesababisha vyama vya kisiasa vya upinzani na wanaharakati kuungana na kupinga hatua zozote za kuchelewesha uchaguzi kupita muda ulowekwa na katiba yani kabla ya mwishoni ma mwaka huu.
Viongozi wa vyama vyote vya upinzani katika hatua nadra walikutaka katika makao makuu ya chama cha MLC na kutowa taarifa ya pamoja kutuhumu serikali kupanga njama ya kutaka kuchelewesha uchaguzi.
Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu mkuu wa chama cha MLC Thomas Luhaka amesema, mbali na tatizo la ratiba inaonekana kuna tatizo la fedha na mwenyekiti wa CENI kasisi Daniel Ngoy Mulunda hakufafanua vyama matatizo yaliyopo katika kuyatayarisha uchaguzi huo.
Kwa upande wake muungano wa vyama tawala PPRD unadai kwamba upinzani unataka mambo yafanyike kwa haraka wakati serikali inataka uchaguzi ufanyike kwa utaratibu na kufuata katiba.
Seenta Mulaila Engabanzo wa muungano wa rais anasema mataifa fadhili yako tayari kugharimia uchaguzi na mipanmgo iko tayari kwa uchaguzi kufanyika kwa muda utakaowekwa.