Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:02

DRC imeishtaki Rwanda kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa


Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi (kushoto) na rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia)
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi (kushoto) na rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia)

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi anataka umoja wa mataifa na ulimwengu kwa jumla kuchukua hatua za dharura na kali kuiwajibisha serikali ya Rwanda, akisema ndio inachangia pakubwa kuvuruga amani mashariki mwa DRC.

Tshisekedi ameambia umoja wa ulaya kwamba licha ya Rwanda kutajwa kila mara katika vita vya DRC, inaendelea kutoa silaha na msaada wa kijeshi kwa kundi la waasi la M23 na kukiuka mikataba yote ya kimataifa Pamoja na maamuzi ya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika mashariki na SADEC.

Katika hotuba iliyojaa ushawishi na kulenga umoja wa mataifa moja kwa moja, mbele ya viongozi wengine kutoka kote duniani kwenye kikao ya 77 cha umoja wa mataifa mjini New York, rais Tshisekedi amelenga utawala wa rais wa Rwanda Paul Kagame, na kueleza ulimwengu namna nchi hiyo, Jirani wa DRC inavyovuruga usalama katika mikoa ya mashariki ya Ituri, Kivu kaskazini na kivu kusini, katika vita ambavyo vimedumu zaidi ya miaka 20.

“Rwanda ndiye mhusika mkubwa katika vita nchini mwangu”

Tshisekedi, amesisitiza kwamba wakati ulimwengu unapambana na ugaidi na vita vinginevyo, majirani wa DRC ikiwemo Rwanda wanaunga mkono makundi ya waasi wakiwemo waasi wa M23 kupiga vita serikali ya DRC, hawaheshimu mfumo wa sheria, hawaheshimu mpaka wa DRC, na wanaiba mali za DRC.

Isitoshe, licha ya kuwepo juhudi za umoja wa mataifa, umoja wa Afrika, jumuiya ya Afrika mashariki, Umoja wa ulaya, muungano wa Sadec, miongoni wa washirika wengine kutafuta suluhu la kudumu nchini DRC, Rwanda imekataa kuheshimu juhudi hizo.

Ameishitaki Rwanda moja kwa moja kwa umoja wa mataifa, akisema inaunga waasi wa M23 kwa kuwapa silaha na msaada wa kijeshi, na hata kuua wanajeshi wa umoja wa mataifa.

“Kundi la waasi la M23 likisaidiwa na Rwanda hata lilipiga na kuangusha ndege ya jeshi la amani la umoja wa mataifa MONUSCO na kuua wanajeshi 8. Kwa kufanya hivyo, walitenda uhalifu wa kivita.”

Juhudi za kuleta amani DRC zimekosa kufanikiwa

Rais Tshisekedi ameeleza juhudi zote ambazo DRC imechukua kuleta amani mashariki mwa DRC lakini zimefeli, akilaumu majirani wake. Miongni mwa juhudi hizo ni kusaini mikataba ya amani, ikiwemo ile ambayo imesimamiwa na jumuiya ya kimataifa, kikanda na umoja wa Africa lakini imekuwa imevunjika baada ya miezi michache ya kusainiwa.

Amesema amechukua juhudi la kibinafsi kuwashirikisha majirani wake katika kuleta amani DRC lakini juhudi hizo zimefeli na kwamba licha ya juhudi zake zote, majirani wake, akiwa na maana Rwnada, wanaendelea kuivuruga na kuivamia DRC kwa kutumia makundi ya waasi, akisisitiza kwamba iwapo Rwanda haitaajibishwa kimataifa, itaendelea na uchukozi huo na kupelekea uhalifu wa kivita ndani ya DRC.

Watu wa DRC watapigania nchi yao kwa kila hali

Tshisekedi amesisitiza kwamba watu wa DRC wataendelea kulinda mipaka yao kwa kila hali, na kwamba hakuna semi za chuki, kikabila au mauaji ya kikabila zitaruhuiwa. Ameongezea kwamba hakuna siku mauaji ya halaiki ya watu yatatokea DRC.

Anataka Umoja wa mataifa kuthathmini pendekezo lake la kutaka kuondoa wanajeshi wake nchini DRC na kutaka vikwazo vya sialaha na kijeshi vilivyowekewa DRC kuondolewa.

“Rwanda huwa inatumia kisingizo cha kundi la waasi la FDLR kushambulia DRC. kundi la FDLR limeisha nguvu. Haya ni madai yasiyokuwa na msingi wowote. Jeshi la DRC lilipiga na kushinda nguvu FDLR na kuwarejesha makwao waliosalia Pamoja na familia zao. Nani amewahi kuona mwanajeshi wa DRC kwenye ardhi ya Rwanda? Hao wapiganaji wa FDLR Wapo sehemu gani ya DRC? Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika na washirika wa DRC wasiendelee kuamini uongo wa Rwanda na badala yake wasaidiwa kujenga usalama wa kudumu wa DRC” amesema rais Tshisekedi

Kiongozi huyo ameeleza umoja wa mataifa kwamba Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeapa kumaliza kabisa ukosefu wa usalama mshariki mwa nchi kwa kutumia kila mbinu na kwamba mda umefika wa kuvunja mikakati yote ya ukosefu wa usalama na kuhakikisha kwamba eneo la maziwa makuu lina usalama na linafaidhika na ukuaji wa uchumi.

Rwanda imekuwa ikikana madai ya kuvuruga usalama wa DRC licha ya tuhuma za kila mara na ripoti za mashirika mbalimbali na za kijasusi.

XS
SM
MD
LG