Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:10

Dr. Conrad Murray akutwa na hatia katika kesi ya Michael Jackson.


Dr. Conrad Murray akiwa mahakamani katika kesi ya kifo cha mfalme wa Pop Michael Jackson.
Dr. Conrad Murray akiwa mahakamani katika kesi ya kifo cha mfalme wa Pop Michael Jackson.

Dr. Conrad Murray akutwa na hatia katika kesi ya Michael Jackson kuuwa bila kukusudia.

Mahakama moja huko Los Angeles California imemhukumu Dr. Conrad Murray kwa kuuwa bila kukusudia katika kesi ya kifo cha Juni 2009 cha mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson.

Jopo la majaji 12 lilifikia maamuzi ya hukumu yake jana baada ya mashauriano yasiyozidi siku mbili. Kesi hiyo ilikuwa ya wiki kadhaa huku karibu mashahidi 50 wakiitwa kwenye mahakama. Mamia ya watu wengi wao wapenzi wa hayati mwanamuziki huyo walijipanga nje ya mahakama hiyo wakati hukumu ikitangazwa na kushangilia uamuzi huo.

Murray alishitakiwa kwa kumpa Michael Jackson dawa kali ya Propofol ili kumsaidia kupata usingizi na kushindwa kumsimamia afya yake. Walisema Murray alishindwa kuwa na vifaa ambavyo vingeweza kuokoa maisha ya mwanamuziki huyo.

XS
SM
MD
LG