Bilionea Donald Trump ambaye anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha Republican amewabeza wapinzani wake wawili kutaka kuvuruga juhudi zake na kusema hatua hiyo " ni kitendo cha hali ya kukata tamaa".
Wapinzani wa Trump, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Gavana wa Ohio, John Kasich, wametangaza mpango huo Jumapili usiku kujaribu kumnyima fursa Trump, ambaye hawajahi kushika wadhifa wa kuchaguliwa, ili asishinde uteuzi katika upigaji kura wa kwanza wa chama utakaofanyika kwenye mkutano wa ktiaifa wa Republican mwezi July, kwa matumaini kuwa wajumbe watawachagua wao katika upigaji kura utakaofuata.
Trump amekejeli juhudi za Cruz na Kasich akisema, "inasikitisha sana kwamba wanasiasa wawili watu wazima wanapanga dhidi ya mtu mmoja ambaye amekuwa mwanasiasa kwa miezi 10 tu ili kujaribu kumzuia mtu hiyo kupata uteuzi wa Republican."