Wafanyakazi wengine kumi na moja waliripotiwa kupotea. Meli hiyo yenye bendera ya Uturuki ya Kafkametler ilizama Jumapili baada ya kugonga kivukio nje ya bandari karibu na mji wa Eregli, takriban kilomita 200 mashariki mwa Istanbul.
Waziri wa uchukuzi na miundombinu Abdulkadir Uraloglu amesema meli hiyo iliyokuwa ikielekea katika bandari ya magharibi ya Uturuki ya Izmir, ilipata dhoruba baharini mara kadhaa kabla ya kuzama.
Shughuli ya utafutaji na uokoaji ilichelewa kwa saa kadhaa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
Lakini hali ilipopungua, waokoaji Jumatatu walipata mwili wa mpishi wa meli hiyo, Uraloglu alisema.
Forum