Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 12, 2024 Local time: 22:01

Darfur imepata kiwango cha msaada kupitia mpaka wa Adre kutoka Chad


Mfano wa malori ya msaada wa kibinadamu katika mpaka wa Adre uliopo kati ya Chad na Sudan. Aug. 21, 2024.
Mfano wa malori ya msaada wa kibinadamu katika mpaka wa Adre uliopo kati ya Chad na Sudan. Aug. 21, 2024.

Malori 15 yamevuka na kuingia Sudan, kati ya malori 131 yaliyobeba chakula cha msaada.

Kiwango kidogo cha misaada kimepitia mpaka wa Adre kutoka Chad na kuingia Dafur, ambayo imekumbwa na njaa. Hii ni baada ya jeshi la Sudan kuondoa marufuku ya kuingia msaada sehemu hiyo, kwa mauda.

Jeshi la Sudan linadhibithi sehemu kubwa ya Darfur na kivuko cha Adre katika vita vya miezi 16. Jeshi lilikuwa limeyaamuru mashirika ya misaada kutotumia kivuko cha Adre tangu mwezi Februari, likisema kwamba kivuko hicho kilikuwa kinatumika kusafirisha silaha, lakini amri hiyo iliondolewa kwa muda wiki iliyopita, na kivuko kitatumika kwa muda wa wiki tatu.

Malori 15 yamevuka na kuingia Sudan, kati ya malori 131 yaliyobeba chakula cha msaada. Shirika la chakula duniani limesema kwamba msaada ambao umeingia Sudan ikiwemo mtama, mafuta ya kupikia na mchele, unatosha watu 13,000. Msaada unaelekea Kreinik, magharibi mwa Darfur.

Forum

XS
SM
MD
LG