Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 11:46

Dada wa rais wa Korea Kaskazini atoa onyo kwa mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini


Kim Yo Jong, dada mwenye nguvu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesema mazoezi ya karibuni ya kijeshi ya Korea Kusini karibu na mpaka kati ya mataifa hayo mawili ni uchochezi usio fichika na wazi, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya serikali KCNA ya Jumatatu.

Kim Yo Jong pia amemshutumu Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol kwa kuanzisha mvutano kwenye rasi ya Korea ili kuhamisha taharuki kwa umma kutokana na utendaji wake mbaya katika siasa za ndani.

Alitoa mfano wa ombi la mtandaoni la kutaka Yoon ashtakiwe, likiwa na sahihi zaidi ya milioni 1. Kim amesema iwapo Korea Kaskazini itahukumu uhuru wake kama ulivyokiukwa, majeshi yake yatatekeleza mara moja oparesheni kwa mujibu wa katiba yake.

Jeshi la Korea Kusini limeanza tena mazoezi ya kurusha risasi karibu na mpaka wa baharini wa magharibi mwishoni mwa Juni, ikiwa mara ya kwanza toka 2018.

Forum

XS
SM
MD
LG