Milio ya bunduki ilisikika kwenye mji mkuu wa Congo, Kinshasa usiku wa kuamkia Jumanne baada ya muda wa Rais Joseph Kabila kuhudumu kama Rais kumalizika bila yake kujiuzulu kama walivyodai wapinzani wake. Muda wa kabila kikatiba ulimalizika saa sita za usiku baada ya muhula miwili madarakani lakini makubaliano ya awali ya kisiasa yameweza kusogeza mbele uchaguzi mkuu hadi mwaka 2018. Mshauri wa Rais Barnabe Kikaya alisema ni kinyume cha katiba kushinikiza Rais kuondoka madarakani usiku wa manane akisema kuwa ataendelea kuwa Rais hata baada ya kupambazuka. Mahakama ya katiba ya DRC tayari imeamua kuwa Kabila anaweza kubaki madarakani hadi pale uchaguzi utakapofanyika. Baadhi ya wakazi wa Kinshasa walipiga filimbi saa sita usiku kuashiria kuwa wakati wa Kabila wa kuondoka ulikuwa umefika. Mapema Jumatatu, maandamano yalishuhudiwa kwenye viunga vya Kinshasa licha ya kupigwa marufuku na kuwepo kwa maafisa wa kijeshi
Milio ya bunduki ilisikika kwenye mji mkuu wa Congo, Kinshasa usiku wa kuamkia Jumanne baada ya muda wa Rais Joseph Kabila kuhudumu kama Rais kumalizika bila yake kujiuzulu kama walivyodai wapinzani wake.