Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 07:21

Comoro wakubaliana ratiba ya uchaguzi


Wananchi wa Comoro wakiwa katika uchaguzi
Wananchi wa Comoro wakiwa katika uchaguzi

Viongozi wa kisiasa Comoro wamekubaliana kuhusu ratiba ya uchaguzi mpya na Sambi abaki kama rais wa kipindi cha mpito.

Sikiliza:

Comoro wakubaliana ratiba ya uchaguzi

Viongozi wa kisiasa katika visiwa vya Comoro wamepata maafikiano kuhusu ratiba ya uchaguzi mpya katika jaribio la kumaliza miezi kadha ya mvutano wa kisiasa nchini humo.

Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Umoja wa Afrika yanamruhusu Rais Ahmed Abdallah Sambi kubaki madarakani kama rais wa mpito mpaka rais mpya atakapochaguliwa baadaye mwaka huu. Raundi ya kwanza ya uchaguzi imepangwa kufanyika Novemba 7 na raundi ya pili itakuwa Disemba 26.

Rais Sambi na magavana wa visiwa vya Ngazidja na Anjouan walitia saini makubaliano hayo Jumatano usiku. Mjumbe maalum Francisco Maderira alitia saini kwa niaba ya Umoja wa Afrika. Gavana wa kisiwa cha Mohali anatazamiwa kuweka saini yake baadaye.

Muda wa Rais Sambi ulimalizika Mei 26 baada ya mahakama ya katiba kufuta sheria iliyoruhusu aendelee kuwa madarakani.

Kulingana na katiba ya Comoro, urais wa taifa hilo lenye visiwa vitatu sasa unatakiwa uende kwa mgombea kutoka kisiwa cha Mohali.

XS
SM
MD
LG