Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:59

Ushindi wa Demokrasia Comoros


Vyama vya upinzani huko Comoros vimepongeza uwamuzi wa mahakama ya katiba wa kumamirsha rais Ahmed Abdallah Sambi kuondoka baada ya mhula wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. Mandamano ya kuunga mkono uwamuzi huo wa kihistoria yamekua yakifanyika visiwani humo.

Vyama vya upinzani na wananchi wa visiwa vya Comoros wamekua wakisherekea uwamuzi wa mahakama ya katiba unaoeleza kwamba Rais Ahmed Abdallah Sambi hana haki ya kuongeza muda wa mhula wake kufuatana na katiba ya nchi hiyo. Hata hivyo mahakama hiyo imesema Rais Sambi atabaki kama Rais wa muda hadi kutayarishwa kwa uchaguzi mpya.

Msemaji wa upinzani Ali Houmadi Msaidie akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Moroni, anesema huo ni uwamuzi muhimu ambao unaonesha kwamba mahakama ya katiba imefikia kiwango cha kua huru na kutopendelea upande wowote. Amesema uwamuzi huo utaimarisha utawala wa kisheria, demokrasia na usalama wa visiwa hivyo.

Bw Houmadi Msaidie amesema "upinzani umefurahi sana kutokana na uwamuzi huo, kwani mapema mwaka huu bunge jipya la Comoros liliidhinisha mswada unaomuongezea Rais Sambi muda wa miezi 18 madarakani na kusababisha wasi wasi wa kisiasa na kuhatarisha usalama wa visiwa hivyo.Kwa hivyo ni ushindi kwa demokrasia na ushindi kwa wakomoro wote".

Msemaji wa upinzani amesema hivi sasa wanasubiri uwamuzi wa Rais na hasa majadiliano yaliyoanzishwa na wapatanishi wa kimataifa ya kumtaka Rais kufikiria upya uwamuzi wake wa kubaki madarakani. Anasema kufuatana na katiba baada ya muda wa mhula kumalizika na ikiwa hakuna uchaguzi ulopangwa basi Rais ana muda wa siku 60 kuitisha uchaguzi.

Kufuatana na katiba ya Comoro, Rais anaruhusiwa kubaki madarakani kwa mhula mmoja wa miaka minne, na kuzunguka kwa zamu kati ya visiwa vitatu, na hivyo zamu hivi sasa ni kwa kisiwa kidogo cha Mwali kumchagua Rais.

XS
SM
MD
LG