Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:50

Clinton na Trump wajiandaa kwa mdahalo wa mwisho kabla ya uchaguzi


Maandalizi ya mwisho ya mdahalo katika chuo kikuu cha Nevada kati ya Donald Trump na Hillary Clinton.
Maandalizi ya mwisho ya mdahalo katika chuo kikuu cha Nevada kati ya Donald Trump na Hillary Clinton.

Mdemokrat Hillary Clinton na Mrepublikan Donald Trump wanakutana katika mdahalo wa tatu na wa mwisho Jumatano huko Las Vegas ,Nevada Trump yuko nyuma ya Clinton katika uchunguzi wa kura za maoni na mdahalo wa Jumatano utakuwa ndio nafasi yake ya mwisho kubadili muelekeo wa uchaguzi ikiwa ni chini ya wiki tatu kufikia siku ya uchaguzi.

Uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni uliofanywa na Real Clear politics unamwonyesha Hillary Clinton akiongoza kwa asilimia 6.4. Clinton pia anaongoza katika majimbo kadhaa muhimu licha ya kura za maoni za CNN za hivi karibuni katika majimbo ya Nevada,North Carolina na Ohio yanaonyesha ushindani mkali licha ya matatizo ya kisiasa yaliomkuta Trump hivi karibuni.

Trump ameendelea kuwaambia wafuasi wake kwamba wanapambana na mashine ya kisiasa ya Clinton na vyombo vya habari vyenye upendeleo. Aliwaambia wafuasi katika mkutano wa kisiasa huko Bangor, Maine, kwamba wana mapambano makali mpaka siku ya uchaguzi.

XS
SM
MD
LG