Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:17

Hillary Clinton kukubali uteuzi wa kihistoria


Hibsga olingan "Reuters" muxbirlarining oila a'zolari hukm o'qilishidan avval Oliy sudga keldi. Yangon, Myanma
Hibsga olingan "Reuters" muxbirlarining oila a'zolari hukm o'qilishidan avval Oliy sudga keldi. Yangon, Myanma

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton, Alhamisi usiku alitazamiwa kuingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa mwanmke wa kwanza kukubali uteuzi wa moja ya vyama vikuu Marekani kugombea kiti cha urais wa Marekani.

Aidha Bi Clinton alitazamiwa kutoa hotuba katika ukumbi wa Wells Fargo mjini Philadelphia, jimbo la Pennsylvania, kuelezea ni kwa nini anaamini kuwa ndiye anafaa kuwa rais kumshinda mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, kupitia tikiti ya chama cha Demokratik.

Siku ya Jumatano, rais Barack Obama wa Marekani alitoa mojawapo ya hutuba za kusisimu kumunga mkono Bi Clinton katika siku ya pili ya mkutano huo mkuu wa chama.

Obama alishangiliwa kwa vifijo na nderemo aliposema: "hapajakuwepo mwanamume wala mwanamke mwenye sifa na uwezo wa kua rais kuliko Hillary Clinton."

Kiongozi huyo alikua anawahutubia wajumbe wa chama cha Demokratik na taifa nzima kwa ujumla juu ya uwezo na sifa za mgombea kiti wa chama cha Demokratik, akisema anafika mwisho wa utawala wake bila ya kukamilisha mengi aliyotaka kufanya na hivyo inabidi Wamarekani wamchaguwe Hillary ambae anauwezo wa kuendeleza mipango yake.

Rais Obama alifafanua nukta moja baadaa ya nyingine juu ya uwezo wa mgombea huyo na kueleza kwamba anawakilisha tabaka zote za wamarekani.

Wengine walio maarufu katika chama cha Demokratik waliotoa hotuba za kusisimua ni pamoja na makamu wa rais Joe Biden na mgombea mwenza wa Bi Hillary Clinton, Tim Kaine. Meya wa zamani wa mji wa New York, Rudy Guilliani, pia alitoa hotuba iliyosubiriwa na wengi hususan kwa sababu yeye anegemea mrengo wa katikati na kufuata sana sera za chama cha Independent.

"Mimi ni mkaazi wa New York...na ninapomuona mtu muongo, mimi humjua mara moja," alisema Gulliani bila kufafanua.

XS
SM
MD
LG