Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:56

Clinton na Trump uso kwa uso kwenye mdahalo wa kwanza wa urais Marekani


Wagombea urais Marekani, Donald Trump (L) na Hillary Clinton huko Hempstead, New York, Sept. 26, 2016.
Wagombea urais Marekani, Donald Trump (L) na Hillary Clinton huko Hempstead, New York, Sept. 26, 2016.

Mdahalo wa kwanza wa urais nchini Marekani umefanyika Jumatatu usiku. Wagombea urais mdemocrat Hillary Clinton na mpinzani wake mrepublican Donald trump walijibu maswali na kutetea sera zao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba nane mwaka huu.

Hillary Clinton, huko Hempstead, New York, Sept. 26, 2016.
Hillary Clinton, huko Hempstead, New York, Sept. 26, 2016.

Clinton alisema ubaguzi bado ni suala kubwa Marekani. Aliendelea kusema kwamba sote tunatakiwa kurejesha tena uaminifu kati ya jamii na polisi na kupambana na mlipuko wa ghasia za bunduki. Pia Clinton aliahidi atahamasisha mageuzi ya sheria ya uhalifu.

Wakati huo huo Trump alisema pale anapoangalia miji kama Charlote katika jimbo la North Carolina, anafikiri kwamba nchi inahitaji “sheria na amri”. Alisema miji maskini yenye jamii ya wamarekani weusi wanaishi katika maisha ya dhiki. Trump alishauri kurejesha sera za “polisi kumsimamisha mtu na kumhoji pale anapomshuku kwa jambo fulani” ambazo zilitumika huko New York City.

Sheria ya kumsimamisha mtu pale unapomshuku kwa jambo fulani ilielezewa kama kinyume na katiba na ilisitishwa huko New York kwa sababu iliwalenga vijana weusi na walatino.

Donald Trump, Sept 26, 2016
Donald Trump, Sept 26, 2016

Lakini Trump alisema sheria iliondolewa kutokana na jaji anayepinga polisi na ingeweza kurejeshwa kama asingekuwepo meya wa jimbo la New York, Bill de Blasio.

Naye bi.Clinton alitoa wito wa maafisa polisi kupatiwa tena mafunzo kwenye masuala kama vile afya ya akili.

Wagombea wote walikubaliana kwamba watu waliopo kwenye orodha ya ugaidi na watu waliopo kwenye orodha ya kuzuiwa kusafiri wanatakiwa kuzuiwa kumiliki bunduki.

XS
SM
MD
LG