Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:06

Clinton na Trump warudi kwenye kampeni zao za uchaguzi


Wagombea wa urais Marekani walipokuwa kwenye mdahalo wa kwanza wa urais.
Wagombea wa urais Marekani walipokuwa kwenye mdahalo wa kwanza wa urais.

Wagombea urais wa Marekani, Hillary Clinton na Donald trump wamerudi kwenye kampeni zao za urais hapo Jumanne siku moja baada ya mdahalo wao uliokuwa na majibizano ambapo wachambuzi huru wanakubali Clinton alishinda mdahalo huo na kupelekea kuongoza kura za maoni ya kitaifa takribani wiki sita kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba nane.

Utafiti wa kisiasa kabla ya mdahalo ulionesha wagombea hao wawili walikaribiana sana ambapo Clinton alikuwa mbele kwa pointi mbili.

Lakini mchambuzi wa kisiasa Alan Abramowitz wa chuo kikuu cha Emory huko Atlanta na mchambuzi wa kura za maoni Nate Silver wote walisema Clinton ataweza kuongeza pointi mbili zingine baada ya kumjibu Trump kwa ufasaha takribani kwenye mdahalo mzima huku akimshambulia kwa maneno kwamba Trump amekataa kuonesha nakala zake alizolipa kodi ya mapato nchini Marekani, vile vile kushindwa kwake kuwalipa mishahara baadhi ya makandarasi aliowaajiri kujenga uwanja wake wa mchezo wa “golf”, casino pamoja na historia yake ya kuwakejeli wanawake.

XS
SM
MD
LG