Kundi la muungano wa wabunge weusi katika bunge la Marekani limetangaza kumwunga mkono Hillary Clinton katika kuwania uteuzi wa chama cha Demokrat katika uchaguzi ujao nchini Marekani.
Wakizungumza mjini Washington Alhamisi wabunge hao ambao wanajulikana kama Black Congressional Caucus walisema Clinton amekuwa msitari wa mbele kwa miaka mingi kugombania haki na maendeleo ya wamarekani weusi.
Bi. Clinton anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea mwingine wa chama hicho Bernie Sanders katika uchaguzi wa awali wa majimbo yafuatayo ya Nevada na South Carolina, hasa baada ya kushindwa vibaya na Sanders katika uchaguzi wa awali wa jimbo la new Hampshire mapema wiki hii.