Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:48

Chombo cha Orion kinatarajiwa kwenda kuzunguka mwezi na kurejea duniani kwa wiki sita


Roketi ya kisasa ya NASA, ikiwa na wafanyakazi wa Orion kwenye eneo la urukaji mapema asubuhi huko Cape Canaveral, Florida, Agosti 29, 2022. REUTERS/Steve Nesius.
Roketi ya kisasa ya NASA, ikiwa na wafanyakazi wa Orion kwenye eneo la urukaji mapema asubuhi huko Cape Canaveral, Florida, Agosti 29, 2022. REUTERS/Steve Nesius.

Wahandisi kutoka idara ya Marekani ya masuala ya anga za juu NASA walifanyia kazi masuala kadhaa mapema leo kabla ya uzinduzi uliopangwa wa roketi mpya na chombo kitakacho kuwa na wana anga na kuelekea tena mwezini.

Wahandisi kutoka idara ya Marekani ya masuala ya anga za juu NASA walifanyia kazi masuala kadhaa mapema Jumatatu kabla ya uzinduzi uliopangwa wa roketi mpya na chombo kitakacho kuwa na wana anga na kuelekea tena mwezini.

Timu ya NASA ilikabiliana na hali ya kuchelewa kwa ratiba kutokana na radi iliyokuwa ikipita katika eneo la kusini mashariki mwa jimbo la Florida pamoja na kuwepo kwa tatizo la kuvuja kwa mafuta.

Naibu mkurugenzi wa NASA Jeremy Graeber, amesema Jumatatu kwamba kuanzishwa kwa operesheni hiyo kutafanyika kama ilivyo pangwa, na endapo itashindikana mpango huo utaahirishwa mpaka Ijumaa.

Majaribio yanajumuisha mfumo wa roketi ambao unaelezwa kuwa na nguvu zaidi katika historia ya NASA ambao utakipeleka chombo cha Orion ambacho kwa sasa hakitakuwa na watu katika safari yake.

Chombo cha Orion kinatarajiwa kwenda kuzunguka mwezi na kurejea duniani na safari yake yote inatarajiwa kuchukuwa wiki sita. Kama kitafanikiwa na oparesheni hiyo, wanaanga watakwenda kuzunguka mwezi mwaka 2024 na kufika kabisa katika mwezi hapo 2025.

XS
SM
MD
LG