Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:13

Chombo cha China chatua salama baada kuzuru mwezi


Chombo cha anga za juu cha China cha Chang'e-6 kilipotua kwenye mwezi, Jumanne, Juni 4, 2024. (CNSA/Xinhua via AP)
Chombo cha anga za juu cha China cha Chang'e-6 kilipotua kwenye mwezi, Jumanne, Juni 4, 2024. (CNSA/Xinhua via AP)

Chombo cha anga za juu cha China kimerejea duniani kikiwa na sampuli ya kwanza ya mchanga na mawe kutoka upande wa mbali wa mwezi. Chang’e-6 kilitua Jumatatu jioni kwenye eneo la ndani la Mongolia, kaskazini mwa China.

Chombo hicho kimekamilisha safari ya kihistoria iliyoanza mwanzoni mwa Mei, pale kiliporushwa kwenye jimbo lililopo kisiwani la Hainan. Zhang Kejian ambaye ni mkuu wa Idara ya China ya Anga za Juu amesema kuwa safari hiyo ilikuwa ya kufana, muda mfupi baada ya chombo hicho kutua.

Rais wa China Xi Jinping ametoa ujumbe akisema kuwa safari ya Chang’e-6, ni hatua muhimu kwenye juhudi za China za kuwa taifa lenye nguvu kwenye sayansi na anga za juu. Chombo hicho kilitua Juni 2, upande wa kusini wa mwezi wa South Pole-Aitken Basin, ambako kuna moja wapo ya bonde kubwa zaidi miongoni mwa sayare zilizopo anga ya juu.

Chang’e 6 ni chombo cha pili cha China kuchukua sampuli za mchanga na mawe kutoka mwezini, wakati kile cha Chang’e 5, kikileta sampuli zake ardhini 2005. Safari hiyo ni sehemu ya China ya kushindana na magwiji wa anga za juu kama vile Marekani na China.

Forum

XS
SM
MD
LG