Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 01:05

China yalaumu Marekani kwa mswaada wa Tiktok

Ofisi za Tik Tok huko California baada ya Bunge la Marekani kupitisha mswaada wa kumiliki tik tok.
Ofisi za Tik Tok huko California baada ya Bunge la Marekani kupitisha mswaada wa kumiliki tik tok.

China siku ya Alhamisi ilisema Baraza la Wawakilishi la Marekani  kuidhinishwa mswaada ambao utailazimisha TikTok kuvunja uhusiano na kampuni mama ya China au kupigwa marufuku nchini Marekani kunafuata mantiki ya kijambazi.

App hiyo fupi ya video imepata umaarufu duniani kote lakini umiliki wake na kampuni kubwa ya teknolojia ya China ya ByteDance na madai ya utiifu kwa Chama tawala cha Kikomunisti cha Beijing kumezua wasiwasi katika miji mikuu ya Magharibi.

Siku ya Jumatano, Baraza la Wawakilishi la Marekani liliidhinisha kwa idadi kubwa mswaada ambao uhuenda ukailazimisha TikTok kuachana na kampuni mama au kupigwa marufuku nchini Marekani.

Mswaada huo bado haujapitishwa na baraza la Seneti, ambako unatarajiwa kukabiliwa na mtihani mgumu kuwa sheria.

Mswaada uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Marekani unaiweka Marekani katika upande mwingine wa misingi ya ushindani wa haki na kanuni za kimataifa za kiuchumi na biashara, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Forum

XS
SM
MD
LG