Mwito huo umetolewa Alhamisi katika taarifa ya pamoja katika kipindi cha kukaribia mwisho wa ziara ya Beijing ya rais wa Iran, Ebrahim Raisi, wakati ambapo mataifa hayo mawili yamejihakikishia uhsirika wa karibu katika masuala ya kiuchumi na kisiasa, na kupinga viwango vya nchi za magharibi vya haki za binadamu na demokrasia.
Toka kuchukuwa madaraka ya Afghanistan, Agosti 2021, Taliban imepiga marufuku wanawake na wasichana kusoma katika vyuo vikuu na shule baada ya darasa la sita ambapo pia iliwalazimisha wote walio chaguliwa kuachana na nyadhifa zao ikiwa na nafasi nyingine maarufu.
Taarifa ya China na Iran imewataka watawala wa Afghanistan kuanzisha serekali inayoshirikisha makundi yote na juhudi zinazo kandamiza wanawake. Imeongeza kusema Marekani na washirika wa NATO wanapaswa kulaumiwa kwa hali ya sasa ya Afghanistan.