Nchi hizo mbili zitafanya mazoezi yaliyopewa jina la Eagle Assault, na wanajeshi kutoka pande zote mbili kwa pamoja watafanya shughuli za uokoaji mateka na oparesheni za kukabiliana na ugaidi,” shirika la habari la serikali la China Xinhua limesema.
Kwa pamoja watajifunza utuaji wa usiku, kuvikabili vizuizi vya maji, na kufanya operesheni katika eneo lenye watu wengi,” kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Belarus.
China na Belarus zina historia ya kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi, ambapo tayari zimeshafanya mazoezi manne ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya nchi zote mbili kuanzia mwaka 2011 hadi 2018.
Forum