Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:29

China yasema haina nia ya kuanzisha vita vya biashara


China inasema inaweza kukabiliana na changamoto yeyote
China inasema inaweza kukabiliana na changamoto yeyote

China imesema Jumapili kwamba haina nia ya kuanzisha vita vya biashara na Marekani kwa sababu hatua hiyo itakuwa janga kwa dunia nzima.

Waziri wa biashara wa China, Zhong Shan alisema pembeni ya kikao cha kila mwaka cha bunge la China kwamba “hakuna washindi katika vita vya biashara”. Aliendelea kusema kuwa “China haitarajii kupambana kwenye vita vya biashara, wala China haitaanza vita vya biashara, lakini tunaweza kukabiliana na changamoto za aina yeyote na tutalinda maslahi ya nchi na watu wetu kwa uthabiti.

Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Siku ya alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini maazimio yanayoweka ushuru wa asilimia 25 kwa uingizaji bidhaa za madini ya chuma na asilimia 10 ya ushuru kwa uingizaji Alminium ambapo kodi mpya kwa bidhaa hizo imepangwa kuanza kutumika mapema mwezi huu.

Wawakilishi wa biashara kwa Japan na Umoja wa ulaya-EU walikutana na mwakilishi wa biashara wa Marekani siku ya Jumamosi katika juhudi za kuepuka vita vya biashara kufuatia tangazo jipya la ushuru wa Alminium na chuma lililotolewa na Rais Donald Trump.

XS
SM
MD
LG