Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 02:46

China imekamata wavuvi wa Taiwan


Mkuu wa pwani ya Taiwan Liao Yun-Hung akionyesha namna boti la uvuvi la Taiwan lilivyoakamatwa na meli za China Jumanne Usiku. July 3 2024 AP
Mkuu wa pwani ya Taiwan Liao Yun-Hung akionyesha namna boti la uvuvi la Taiwan lilivyoakamatwa na meli za China Jumanne Usiku. July 3 2024 AP

Mabaharia wa boti ya uvuvi ya Taiwan wamekamatwa baada ya boti yao kukamatwa na walinzi wa pwani ya China, walipokuwa wakifanya shughuli zao karibu na kisiwa kinachodhibitiwa na Taiwan.

Walinzi wa pwani ya Taiwan wamesema kwamba boti hiyo ilikamatwa na meli za China jumanne usiku karibu na kisiwa cha Kinmen, kilicho kilomita chache kutoka mji wa Xiamen, ulio kusini mwa China.

Walinzi wa pwani ya Taiwan wamesema kwamba walituma boti tatu za doria kuwasaidia wavuvi hao, lakini boti zilizuiliwa na meli za tatu za China.

Wamesema kwamba walitaka maafisa wa China kuwaachilia wavuvi na boti zao lakini wakaonywa dhidi ya kuingilia kati.

Walinzi wa pwani wa Taiwan wamesema kwamba waliondoka ili kuepusha kutokea mzozo.

Boti hilo ya uvuvi ilichukuliwa na kupelekwa kwenye bandari ya uvuvi iliyo karibu. Watu watano waliokuwa kwenye boti hiyo ni raia wawili wa Taiwan na watatu wa Indonesia.

Mnamo mwezi Februari, wavuvi wawili wa China walifariki baada ya boti yao kuzama ilipokuwa inawatoroka walinzi wa pwani wa Taiwan. Boti ilikuwa imeingia sehemu ya bahari yenye mzozo, karibu na Kinmen.

Forum

XS
SM
MD
LG