Mazoezi hayo ya kijeshi ni makubwa zaidi kuwahi kufanywa na China, wakilalamikia ziara ya spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi nchini Taiwan.
China imesema kwamba mazoezi yake yataangazia zaidi operesheni ya kijeshi baharini, na hatua hiyo imepelekea hofu kwamba huenda Beijing itaendelea kushinikiza kutaka kuuchukua utawala wa Taiwan.
Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan imeikosoa hatua hiyo ya China, ikisema kwamba ilikuwa inasababisha mgogoro makusudi, na kutaka kuacha mazoezi hayo.