Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:41

China haitaiuzia silaha Russia


Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock huko Beijing tarehe 14 Aprili 2023. Picha na Suo Takekuma / POOL / AFP.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock huko Beijing tarehe 14 Aprili 2023. Picha na Suo Takekuma / POOL / AFP.

China haitauza silaha kwa upande wowote unaohusika katika vita nchini Ukraine, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo alisema siku ya Ijumaa, akijibu wasiwasi wa nchi za Magharibi kuwa Beijing inaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Russia.

China imesisitiza kuwa haiegemei upande wowote katika mzozo huo, huku ikiiunga mkono Russia kisiasa, kiuchumi na katika mazungumzo, wakati ambapo mataifa ya Magharibi yameiwekea vikwazo kuiadhibu na kutaka kuitenga Moscow kwa kumvamia jirani yake.

Qin Gang ambaye ni afisa wa ngazi ya juu sana wa China kutoa taarifa hiyo kiunagaubaga kuhusu suala la kuiuzia silaha Russia. Ameongeza kuwa China pia itadhibiti usafirishaji nje wa bidhaa zinazotumiwa na raia pamoja na wanajeshi.

"Kuhusu mauzo ya nje ya bidhaa za kijeshi, China inachukua mtazamo wa busara na uwajibikaji," Qin alisema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anayetembelea nchi hiyo.

"China haitatoa silaha kwa pande zinazohusika katika mzozo huo, tumeweza kusimamia na kudhibiti usafirishaji wa bidhaa kwa matumizi ya kiraia na kijeshi kwa mujibu wa sheria na kanuni."

Waziri huyo pia alisisitiza nia ya China ya kusaidia kupatikana kwa suluhisho la amani katika mzozo huo.

Mwezi Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema ujasusi wa Marekani unapendekeza kuwa China ina mpango wa kuipa Russia silaha na risasi - alionya kwamba kujihusisha huko katika vita vya Kremlin itakuwa "tatizo kubwa."

Katika siku za hivi karibuni, viongozi wa nchi za Ulaya wametoa maonyo kama hayo, hata wakati walipoitembelea China, na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya aliishutumu Beijing, akisema uungaji mkono wake kwa Russia wakati wa uvamizi ilikuwa ni "ukiukaji wa wazi" wa ahadi zake katika Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG