Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 07:33

Mashambulizi kutoka kwa watu binafsi ni changamoto


Mkurugenzi wa shirika la FBI, James Comey.
Mkurugenzi wa shirika la FBI, James Comey.

Licha ya juhudi zote zilizochukuliwa na Marekani pamoja na mataifa mengine za kukabiliana na ugaidi, shambulizi la Jumapili mjini Orlando, Florida limeonyesha kuwa tishio kutoka kwa watu binafsi bado ni changamoto kubwa kwa serikali.

Mkurugenzi wa shirika la FBI, James Comey, amesema Jumatatu kuwa kufikia sasa hakuna jambo linaloashiria kwamba mshambuliaji alikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kundi la Isamic State, lakini anaamini alipata mafuzo ya kigaidi kupitia mtandao wa internet.

Picha ya ISIS ikiwa na lengo la kusambaza propaganda
Picha ya ISIS ikiwa na lengo la kusambaza propaganda

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa ripoti mapema mwezi huu ikisema kuwa visa vya mashambulizi ya kigaidi ulimwenguni vilikuwa vimepunguka kwa asilimia 13 mwaka jana huku idadi ya vifo ikipunguka kwa asilimia 14.

XS
SM
MD
LG