Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:01

Chama cha wafanyakazi Nigeria chaitisha maandamano


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Chama cha Labour Congress (NLC) cha Nigeria kitaanza maandamano ya siku mbili Julai 26

Chama cha Labour Congress (NLC) cha Nigeria kitaanza maandamano ya siku mbili Julai 26 kupinga kufungiwa kwa vyuo vikuu vya umma kwa muda wa miezi sita kote nchini humo kutokana na kutoelewana kwa malipo kati ya serikali na walimu. kilisema Jumapili.

NLC, chama kikuu mwavuli cha wafanyakazi wa nchi hiyo, kinawakilisha mamilioni ya wafanyakazi katika sekta nyingi za uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, ikiwa ni pamoja na sehemu za sekta ya mafuta. Ilisema katika taarifa yake itawahamasisha wafanyakazi kwa ajili ya maandamano ya utawala bora.

Vifaa vya kufundishia na malipo vimesababisha migomo ya awali dhidi ya serikali ambayo hutoa fedha nyingi kwa shule za umma.

XS
SM
MD
LG