Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 10:55

Chama cha mrengo mkali wa kulia nchini Ufaransa kimepata kura nyingi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge


Wafuasi wa kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia, Marine Le Pen, wakisherekea ushindi wa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge, Juni 30. Picha ya Reuters
Wafuasi wa kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia, Marine Le Pen, wakisherekea ushindi wa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge, Juni 30. Picha ya Reuters

Wapiga kura wa Ufaransa wamekipa ushindi chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge Jumapili na kuiweka nchi katika hali isiyo na uhakika, kulingana na makadirio ya matokeo ya uchaguzi.

Rais Emmanuel Macron, ambaye aliitisha uchaguzi wa kushtukiza wiki tatu zilizopita, aliwataka wapiga kura kuungana dhidi ya chama hicho cha mrengo mkali wa kulia katika duru ya pili ya uchaguzi.

Kiongozi wa chama hicho Marine Le Pen aliwaomba wapiga kura kukipa chama chake cha National Rally “ wingi wa viti katika bunge. Alisema chama chake kikiwa na wabunge wengi kitakuwa na uwezo wa kuunda serikali mpya pamoja na mwenyekiti wa chama hicho Jordan Bardella kama waziri mkuu ili kufanya kazi kuiimarisha Ufaransa.

Makadirio ya taasisi za kura ya maoni yanaonyesha National Rally kina nafasi nzuri ya kushinda wingi wa viti katika bunge kwa mara ya kwanza, na wastani wa theluthi moja ya kura za duru ya kwanza, karibu maradufu ya asilimia 18 ya kura kilizopata katika duru ya kwanza mwaka 2022.

Chama hicho kimeimarisha mafanikio yake katika uchaguzi wa Ulaya ambao ulisababisha Macron kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi huo wa kushtukiza.

Duru ya pili itakuwa ya maamuzi lakini inaacha wazi masuali makubwa kuhusu jinsi Macron atashirikiana madaraka na waziri mkuu ambaye anapinga sera zake nyingi.

Forum

XS
SM
MD
LG