Bunge la Kitaifa limepangwa kuanza Ijumaa ili wabunge waapishwena kumchagua spika mpya, naibu wake na rais.
Hata hivyo, chama cha Umkhonto weSizwe (MK), ambacho kilishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa hivi karibuni, kimewasilisha malalamiko kisheria kuomba mahakama ya kikatiba ya Afrika Kusini kufuta uamuzi wa tume ya uchaguzi wa kutangaza uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
MK, ambacho kinaongozwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kinadai kwamba kulikuwa na dosari katika upigaji kura na kuomba uchaguzi urudiwe.
Forum