Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:49

Chama cha ANC cha Afrika Kusini kinataabika kupata asilimia 50 ya kura


African National Congress (ANC). May 29, 2024.
African National Congress (ANC). May 29, 2024.

Kama chama cha ANC kitashindwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza viti vingi bungeni tangu kumalizika enzi ya ubaguzi wa rangi 1994.

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ambacho kilipata madaraka chini ya Rais Nelson Mandela, kimepata chini ya asilimia 50 ya kura katika matokeo ya awali ya uchaguzi.

Kama ANC kitashindwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza viti vingi bungeni tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Takriban asilimia 27 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Jumatano zimehesabiwa kufikia Alhamisi. Tume huru ya uchaguzi imesema kura za mwisho zitawasilishwa siku ya Jumapili. ANC ina asilimia 43 ya kura zilizotokana na matokeo kutoka kwenye vituo 6,000 kati ya 23,000 vya kupigia kura katika majimbo tisa ya Afrika Kusini.

Kama ANC hakitapata wingi wa viti, kitahitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili kumchagua tena Rais Cyril Ramaphosa kwa muhula wa pili

Forum

XS
SM
MD
LG