Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:40

CDC Africa yaonya dhidi ya kulegeza juhudi za kukabiliana na Covid-19


WHO COVID Africa
WHO COVID Africa

Janga la COVID-19 bado ni tishio katika bara la Afrika, kutokana na viwango vya chini vya chanjo, kaimu mkurugenzi wa kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, (Africa CDC), alisema Alhamisi.

"Virusi bado vinazunguka, na kwa sababu ya viwango vya chini vya chanjo, ugonjwa huo bado uko nasi, hapa barani,"

Ahmed Ogwell Ouma, aliambia mkutano wa wanahabari Alhamisi. Alikuwa akijibu swali kuhusu iwapo, alikubaliana na maoni ya mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tedros Adhanom Ghebreyesus, kwamba mwisho wa janga la COVID sasa unakaribia.

Ouma alisema zaidi ya asili mia 22 ya watu wa Afrika wamechanjwa kikamilifu, dhidi ya COVID na kwamba shirika hilo litaendelea kushinikiza kuongeza idadi hiyo.

Mwanzoni mwa janga la Corona, nchi za Kiafrika zilitatizika kupata vifaa na chanjo ya COVID, huku mataifa tajiri yakihodhi dozi, na hivi karibuni, kusitasita na changamoto za kimikakati zimeifanya vigumu kwa baadhi ya watu barani humo kupata chanjo.

Gebreyesus alisema Jumatano kwamba,katika kipindi cha wiki moja iliyopita, takwimu zilionyesha kuwa idadi ya vifo dunini kutokana na ugonjwa huo, ilishuka kuliko wakati mwingine wowote tangu janga hilo kuripotiwa

XS
SM
MD
LG