Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:23

Raia wa Cameroon waungana kusheherekea mwezi mtukufu wa Ramadhan


Waumini wa kiislamu , Cameroon
Waumini wa kiislamu , Cameroon

Waislamu kote duniani wanaadhimisha mwezi wa Ramadhan kwa kufanya ibada na kufunga. Nchini Cameroon, wakristo na wale wa dini za kienyeji, wanaungana na waislamu kwa mlo wa jioni kuonyesha mshikamano dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulizi upande wa kaskazini tangu mwaka 2014.

Mamia ya watu walikusanyika katika msikiti mkubwa mjini Yaounde kusali na kufuturu. Lakini sio wote ni waislamu. Wakristo nao pia wamekuja kuungana na wenzao. Wanasubiri nje kwenye uwa wakati waislamu wanasali. Charles Nzobo ni mkuu katika kanisa la katoliki hapo mjini.

Bw Nzobo anasema ujumbe ni mmoja. Tuiache Cameroon ibaki kama ilivyokuwa. Wakristo na Waislamu wanapaswa kuishi pamoja. Hatupaswi kubaguana na tunaiombea Camerron izidi kuwa bora.

Cameroon haina historia ya mizozo ya kidini. Lakini baadhi wanahofu kuwa uasi wa Boko Haram upande wa kaskazini unaleta mivutano na mashaka baina ya wakristo na waislamu kama walivyofanya nchini Nigeria.

Takriban robo ya raia wa Cameroon ni waislamu. Maafisa wamewakamata dazeni ya viongozi wa dini ya kiislamu kwa tuhuma kuwa wanaliunga mkono Boko Haram. Lakini wale walokusanyika msikitini wanasema watu hawapaswi kujumuishwa.

Joseph Ndinga, mkuu wa kikabila katika makazi ya kikabila ya Tsibnga Younde, anasema kukusanyika kufuturu pamoja ni kuonyesha mshikamano na jamii ya waislamu ambao watasiaidia mapambano na Boko Haram.

Bw Ndinga anasema, ni utamaduni wa kiafrika. Ikiwa mtu anafurahi au ana maumivu, basi unakwenda kwa kaka yako au dada yako anapofikwa na jambo liwe zuri au baya.

Kwa waislamu, Ramadhan ni mwezi mtukufu sana katika mwaka. Baadhi ya maimamu wanasema ni waislamu pekee walofunga ndio wanapaswa kushiriki katika futari hiyo. Lakini Muhammadou Labarang, katibu wa msikiti anasema watu wote wanakaribishwa.

Anasema wanakula pamoja kwa heshima ya maelekezo ya kuran tukufu kuwa waumini wanapaswa kushirikiana na kupata Baraka kutoka kwa mungu. Anasema anamshukuru mungu kuwa waislamu na wasio islamu wanaweza kuishi pamoja nchini Cameroon na kuwa wanaomba amani.

XS
SM
MD
LG