Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:34

Burundi yatajwa kuongoza kwa rushwa Afrika Mashariki.


Mcheza ngoma asilia wa Burundi.
Mcheza ngoma asilia wa Burundi.

Shirika la Transparency International limesema Burundi imechukua nafasi ya Kenya kama nchi inayoongoza kwa rushwa Afrika Mashariki.

Shirika linafuatilia maswala ya rushwa Transparency International limesema Burundi imechukua nafasi ya Kenya kama nchi inayoongoza kwa rushwa huko Afrika Mashariki.

Transparency International imesema hayo katika ripoti yake ya mwaka 2010 Alhamisi. Ripoti hiyo inahusu utafiti uliowahusisha zaidi ya watu 10,000 katika eneo la Afrika Mashariki na kati, na kubaini kuwa rushwa imeenea zaidi huko Burundi ikifuatiwa na Uganda, Kenya, Tanzania na Rwanda.

Shirika hilo limesema mamlaka ya mapato ya Burundi ndio inaongoza kwa rushwa katika nchi hizo tano, ikifuatiwa na jeshi la polisi la Burundi. Polisi wa Kenya ambao waliongoza katika utafiti wa mwaka 2009 wako katika nafasi ya tatu mwaka huu.

Kwa upande wa habari njema Transparency International inasema matukio ya rushwa ni machache mno nchini Rwanda na wanasema wanatarajia kuwa uchunguzi wa siku zijazo unaweza kuelezea kwa nini.

Shirika hilo limetaja kiwango cha kusambaa kwa rushwa nchini Rwanda kipo katika asilimia 6.6 kinyume na Burundi ambako ilikuwa ni asilimia 36.7

XS
SM
MD
LG