Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 17:53

Burkina Faso inaishutumu Ivory Coast kwa kuwakaribisha wahujumu nchini humo


Ramani ya Burkina Faso na nchi jirani zinazopakana nazo.
Ramani ya Burkina Faso na nchi jirani zinazopakana nazo.

April 19 mawaziri wao wa ulinzi walifanya mkutano kwa lengo la kuleta “mwanzo mpya” katika mahusiano ya nchi hizo mbili.

Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Burkina Faso, Ibrahim Traore, aliishutumu Ivory Coast siku ya Ijumaa kwa kuwakaribisha wahujumu wote wa nchi yake, akiongeza kuwa kulikuwa na tatizo na mamlaka mjini Abidjan.

Hivi karibuni uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiyumba, na Aprili 19 mawaziri wao wa ulinzi walifanya mkutano katika mpaka huo kwa lengo la kuleta “mwanzo mpya” katika mahusiano.

Akiizungumzia Ivory Coast katika mahojiano na kituo cha televisheni cha taifa RTB, Traore alisema “wahalifu wote wapo na hawajifichi”. Ameongezea kuwa kuna wakati, lazima tuache unafiki na kusema ukweli, kuna tatizo na mamlaka ya nchi hii.

Serikali ya Traore ilichukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2022 na tangu wakati huo imejitenga na mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa, ikipendelea mahusiano ya karibu na tawala nyingine za kijeshi katika eneo hilo, pamoja na Russia. Akizungumza kuhusu rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Traore amesema hana mawasiliano maalum na yeye.

Forum

XS
SM
MD
LG