Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:07

Bunge la Uturuki laidhinisha mswaada unaoiruhusu Finland kujiunga na NATO


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Finland Sauli Ninisto wakizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu mjini Ankara, Machi 17, 2023.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Finland Sauli Ninisto wakizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu mjini Ankara, Machi 17, 2023.

Bunge la Uturuki Alhamisi limeidhinisha mswaada wa sheria ili kuiruhusu Finland kujiunga na NATO, na hivyo kuondoa pingamizi zote kwa Helsinki kujiunga na muungano wa ulinzi wa mataifa ya Magharibi wakati vita vikipamba moto nchini Ukraine.

Bunge la Uturuki lilikuwa la mwisho kati ya wanachama 30 wa NATO kuidhinisha uanachama wa Finland baada ya bunge la Hungary kuidhinisha mswaada kama huo mapema wiki hii.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema mapema mwezi Machi kwamba Finland ilipata baraka ya Uturuki baada ya kuchukua hatua madhubuti kutimiza ahadi zake kukabiliana na makundi yanayochukuliwa na Ankara kama makundi ya kigaidi, na kufungua mauzo nje ya nchi ya vifaa vya ulinzi.

Finland na Sweden ziliomba kujiunga na NATO mwaka uliopita kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine. Lakini mchakato huo ulizuiliwa na Uturuki na Hungary. Lazima mabunge ya nchi wanachama wote wa NATO yaidhinishe uanachama wa wanachama wapya.

XS
SM
MD
LG