Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:25

Bunge la Somalia lashambuliwa kwa mizinga


Wabunge wa Somalia, Mogadishu, April 12, 2021.
Wabunge wa Somalia, Mogadishu, April 12, 2021.

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la mizinga dhidi ya bunge la Somalia wakati wabunge walikuwa wakikutana kwa mara ya pili tangu walipoapishwa wiki iliyopita.

Hakuna mbunge amejerihiwa katika shambulizi hilo dhidi ya jengo lenye ulizi mkali sana mjini Mogadishu, na ambalo kundi la kigaidi la Al-shabaab limedai kutekeleza.

Walioshuhudia shambulizi hilo wameambia Sauti ya Amerika VOA kwamba watu saba wamejeruhiwa.

Kati ya waliojeruhiwa ni wafanyakazi wawili wa buge na walinzi watano.

Bunge la Somalia lipo karibu na ikulu ya rais, katikati mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Kikao cha Jumatatu cha mabaraza mawili ya bunge kilikuwa kikipeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni, wakati shambulizi hilo lilipotokea. Wabunge waliambiwa wabaki ndani ya bunge wakati shambulizi lilipotokea.

Wabunge walikuwa wakijadiliana kuhusu tarehe ya kumchagua spika wa mabaraza mawil ya bunge, kabla ya kumchagua rais.

Kikao hicho cha bunge kimekubaliana kumchagua spika wa baraza dogo hapo April tarehe 26, huku wa baraza kuu akipangiwa kuchaguliwa April 27, na baadaye kuandaliwa uchaguzi wa Rais baada ya Ramadhan.

Kundi la kigaidi la Al-shabaab, lenye ushirikiano na kundi la Al-Qaeda, limekuwa likitekeleza mshambulizi ya kila mara dhidi ya serikali kwa zaidi ya mwongo mzima.

Kikosi cha umoja wa mataifa, cha kulida usalama nchini Somalia UNSCOM, kimtoa taarifa inayokemea vikali shambulizi hilo, na kusema kwamba inaunga mkono juhudi za Somalia kuandaa uchaguzi na kulinda maslahi ya taifa.

Baadhi ya viti vya bunge havijajazwa, lakini wabunge 297 kati ya wabunge 329 wameapishwa siku ya alhamisi.

Somalia haijawahi kuandaa uchaguzi wa kawaida wa raia kuwachagua viongozi wao, katika kipindi cha miaka 50.

XS
SM
MD
LG