Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:32

Bunge la Israel limekataa pendekezo la kuundwa kwa taifa la Palestina


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipohudhuria mkutano na waandishi wa habari Tel Aviv Oktoba 28, 2023 Picha na Abir SULTAN / POOL / AFP
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipohudhuria mkutano na waandishi wa habari Tel Aviv Oktoba 28, 2023 Picha na Abir SULTAN / POOL / AFP

Bunge la Israel limepiga kuunga mkono wazo la waziri mkuu Benjamin Netanyahu la kupinga kuundwa kwa taifa huru la Wapalestina.

Pendekezo hilo limetolewa na viongozi mbali mbali duniani wanaotaka juhudi zifufuliwe za kufikia suluhisho la mataifa mawili kwa lengo la kumaliza mgogoro wa miongo kadhaa kati ya Israel na Palestina.

Chama cha Likud, cha Netanyahu, kimesema kwamba wabunge 99 kati ya 120 wamepiga kura kuunga mkono maamuzi ya baraza la mawaziri yaliyofikiwa wiki hii.

Msimamo wa Israel ni kwamba mkataba wowote wa kudumu kati yake na Palestina unastahili kupitia mchakato wa mazungumzo kati ya pande hizo na wala sio kwa shinkizo la kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG