Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:19

Bunge la Ethiopia laidhinisha uteuzi naibu waziri mkuu

Bunge la Ethiopia lilipomuapisha Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa muhula wa pili wa miaka mitano Oktoba. 4, 2021.
Bunge la Ethiopia lilipomuapisha Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa muhula wa pili wa miaka mitano Oktoba. 4, 2021.

Bunge la Ethiopia Alhamisi liliidhinisha uteuzi wa mkuu wa idara ya ujasusi Temesgen Tiruneh kama naibu waziri mkuu, akichukua nafasi ya Demeke Mekonnen, ambaye alihudumu katika jukumu hilo kwa miaka 11, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Aidha, bunge lilikubali uteuzi wa Taye Atske Selassie, balozi wa zamani katika Umoja wa Mataifa, kuwa waziri wa mambo ya nje. Demeke pia alihudumu kama waziri wa mambo ya nje tangu mwaka 2020.

Temesgen, ambaye ameratibu majibu ya serikali kwenye mzozo uliozuka mwaka jana katika eneo la Amhara, alichaguliwa mwishoni mwa Januari kumrithi Demeke kama makamu wa rais wa chama tawala- Prosperity Party.

Makamu wa rais wa chama kwa kawaida huchukua jukumu la naibu waziri mkuu.

Demeke amekuwa uso wa mwendelezo wakati wa msukosuko katika siasa za Ethiopia. Aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu baada ya kifo cha waziri mkuu wa muda mrefu Meles Zenawi mnamo mwaka 2012 na aliendelea kubaki wakati wa kupangwa upya kwa safu ya uongozi kwenye chama tawala baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuingia madarakani mwaka 2018.

Forum

XS
SM
MD
LG