Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 17, 2025 Local time: 02:52

Bunge jipya la Msumbiji laapishwa Jumatatu


Wabunge wa Msumbiji kutoka chama tawala cha Frelimo wakiwa kwenye hafla ya kuapishwa Jumatatu mjini Maputo, Jan. 13, 2025.
Wabunge wa Msumbiji kutoka chama tawala cha Frelimo wakiwa kwenye hafla ya kuapishwa Jumatatu mjini Maputo, Jan. 13, 2025.

Bunge jipya la Msumbiji limekutana Jumatatu kwenye mji mkuu , ambapo wabunge 210 walikula viapo vyao huku vyama vya upinzani vikisusia na kuendelea na maandamano baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni. 

Magari ya kijeshi pamoja na polisi wa kijeshi walizingira jengo la bunge huku polisi wakifunga bara bara zote kuelekea huko wakati wa hafla hiyo mjini Maputo. Usalama uliimarishwa kote mjini humo ambao kwa kawaida huwa na shughuli nyingi Jumatatu, huku maduka yakibaki yamefungwa baada ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani aliyeshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa rais Venancio Mondlane, kufunga barara kuelekea kwenye maeneo kadhaa.

Mondlane ambaye ni maarufu miongoni mwa vijana, anashikilia kuwa uchaguzi huo uliibwa na kupendelea chama tawala cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 50. Mwishoni mwa wiki, aliomba wafuasi wake waendelee kukataa matokeo ya uchaguzi kuanzia Jumatatu hadi Jumatano, siku ambayo rais mteule Daniel Chapo amepangwa kuapishwa.

Vyama vingine viwili vidogo vya upinzani ,Renamo na Mozambique Democratic Movement pia vilisusia hafla hiyo, vikisema kuwa vinapinga matokeo ya uchaguzi huo wa Oktoba. Chama cha PADEMOS chake Mondlane kinaingia kwenye bunge la kitaifa kwa mara ya kwanza. Kiongozi wa chama hiicho Abino Forquilha akiwa kwenye lango la kuingia bungeni alisema kuwa yupo tayari kukabiliana na utawala wa Frelimo wa chama kimoja.

Forum

XS
SM
MD
LG